Safari za Hija na Umra kwa Elimu na Utulivu

Tunawaongoza Waumini wa Tanzania na Zanzibar kutekeleza Hija na Umra kwa elimu sahihi ya ibada, ratiba iliyoandaliwa vizuri, na mazingira ya utulivu yanayokuwezesha kuzingatia ibada kikamilifu.

kuhusu taasisi yetu

Zanzibar Istiqaama Hajj and Travelling Agency (Istiqaama Mothercare) ni moja kati ya taasisi inayoandaa Safari za Hajj kwa muda mrefu zaidi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, tangu mwaka 2001. Huduma zetu kwa mahujaji pamoja na bei nafuu zimetupatia umaarufu na kuaminika katika jamii yetu. Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa tayari imeshasafirisha takriban mahujaji 3500 , ambao kwa uwezo wa Allah tumewasaidia kutekeleza ibada ya Hijja.
Mpangilio na maelekezo ya ibada ya hajj kutoka kwa Wasomi wetu wa dini, Viongozi wa taasisi na Madaktari wanahakikisha kuwa Hujaji amejitayarisha vyema kabla ya Hijja, na wakati wa Hijja humuongoza kwenye Ziara yenyewe ya Hajj katika hali bora na utulivu.. Soma Zaidi

Safari Zetu Maalum za Hija na Umrah.

HIJA CLASS D 2026

Safari ya Hija iliyoandaliwa kwa umakini ikijumuisha safari ya ndege, hoteli za nyota 5 Madina na Makkah, treni ya Economy Class, makazi ya Mina na Arafat Class D, elimu ya Hija na uangalizi wa karibu wa mahujaji.
$6,500

UMRAH YA RAMADHANI 2026

Safari maalum ya Umrah katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikijumuisha hoteli Madina na Makkah, futari na daku, pamoja na uongozi wa kiibada kwa kipindi chote cha safari. Vifurushi kuanzia USD 3,900
$ 3,900

Jisajili Sasa kwa Hija & Umrah 2026

Usikose fursa ya kutekeleza ibada yako tukufu kwa elimu, utulivu, uaminifu na uongozaji wa kitaalamu. Istiqaama Mothercare ipo tayari kukusimamia safari yako kuanzia maandalizi hadi kurejea salama.

Wasiliana Nasi

Tupo Karibu Nawe – Popote Ulipo

Ofisi Kuu (Unguja – Zanzibar)

📍 Vikokotoni, Zanzibar
📞 0777 422 838
📞 0776 829 044
📲 WhatsApp: 0773 047 979
✉️ zihatavikokotoni@yahoo.com

Huduma kamili za usajili wa Hija & Umrah

Ofisi zetu nyengine

📍 Ofisi ya Pemba

📞 0777 415 456
📞 0777 428 898

 

📍 Ofisi ya Dar es Salaam

📞 0773 271 929
📞 0713 604 658

 

 

Maelezo Muhimu

Tarehe za Safari

Safari ya Hija: Kuondoka Mei 16, 2026 – Kurudi Juni 6 2026

Safari ya Umra ya Ramadhani: Kuondoka Machi 6, 2026 – Kurudi Machi 16 2026

Pakua Ratiba ya Semina za Hija
Ratiba Ya Semina 2026

Pakua Fomu ya Usajili

Fomu 

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَأَذِّن فِى ٱلنَّاسِ بِٱلْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًۭا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍۢ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍۢ

Quran 22:27- Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.

Tafsir— Ali Muhsin Al-Barwani.